Categorized | Swahili, WSF 2011

Kongamano la Kijamii la Dunia: Wakenya Wanawasha Moto Mwingine

Posted on 06 February 2011 by editor

Paulino Menezes/IPS TerraVivaSherehe za Ufunguzi wa Kongamano la Kijamii la Dunia Mjini Nairobi. Kutoka kwa: Paulino Menezes/IPS TerraViva

Paulino Menezes/IPS TerraVivaSherehe za Ufunguzi wa Kongamano la Kijamii la Dunia Mjini Nairobi. Kutoka kwa: Paulino Menezes/IPS TerraViva

Na Mary Itumbi

NAIROBI, Feb 3 (IPS) – “Miongoni mwa mambo ambayo tutayapeleka Dakar, anasema Onyango Oloo, “ni [ujuzi wa] kukosa uwezo wa kuandaa Kongamano la Jamii la Dunia.” Oloo alikuwa mratibu wa Kongamano la Jamii Duniani (WSF) lilipofanyika jijini Nairobi mwezi Januari 2007, na kuwa wa kwanza kugundua mikanganyiko  iliyoizunguka kongamano la kwanza la WSF kufanyika barani Afrika.

“Wakati huo huo tungependa kukumbuka kwamba Kongamano la Kijamii la Dunia lilikuwa kubwa kulikoni yote katika ardhi ya Kenya kuhusiana na uwakilishi wa jamii. Liliamsha hamasa nyingi, hata (kutoka) makundi mengine ya kijamii hususan mashoga, wasagaji, wanaopenda jinsi zote mbili, wanaharakati wote. Walizindua kwa mara ya kwanza, walisimika hema lao kubwa (katika eneo la kongamano) katika uwanja wa Karasani, mambo mengi ya kusisimua yalitokea.”

Zaidi ya watu 200 walihudhuria tukio la awali kabla ya WSF lililotayarishwa na shirika la kijamii la Nairobi Januari 29, kutoka vikundi mbalimbali vya mashirika yanayohusiana na masuala ya haki za binadamu, haki za wazawa, mabadiliko ya hali ya hewa na mengineyo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Ufungamano, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Nairobi.

Lengo la tukio hilo ni kuamsha hamasa za wananachi wa Kenya katika Kongamano la Kijamii la Dunia. Kongamano la mwaka 2007 lilikosolewa kwa uwakilishi wa hali ya juu ya mashirika na vyama vya kimataifa na kiwango cha juu cha gharama ya usajili, na kuwaacha Wakenya wengi walio maskini kushindwa kuhudhuria. Wakenya waliofanya kazi ya kujitolea pia walilalamika kwa kutotendewa haki.

Kwa kutafakari, Oloo anasema kwamba kinachohitajika katika WSF ni uwakilishi mkubwa wa wanaharakati kutoka sekta ya wanajamii wenyewe kuliko mashirika yasiyo ya kiserikali.

“Wanaharakati wa kijamii kwa ujumla wana mtizamo wa kimaendeleo lakini sio wakati wote. Kwa mfano,  [nchini Kenya] tuna wanaharakati wa Mungiki ambao wana wanachama zaidi ya milioni. Wanafanya mambo mazuri lakini wakati mwingine wanajihusisha na vitendo vya kihuni, na wakati mwingine vya kihalifu. Kwa hiyo kikundi cha uanaharakati kwa namna moja au nyingine sio cha kimaendeleo, lakini vikundi vya kijamii ninavyoviongelea ni vile ambavyo vina mwelekeo wa kimaendeleo wa kuibadilisha jamii. Uanaharakati katika sekta zisizo rasmi, za wafanyakazi, vijana na wanawake – hivyo ndivyo vikundi ninavyoviongelea.”

Njoki Njehu ni miongoni mwa wanachama wa  Daughters of Mumbi Resource Centre, kituo cha mtandao wa vikundi vya wanawake vinavojitegemea vinavyofanya kazi katika masuala ya usalama wa chakula, haki za jinsia, ushiriki wa raia na demokrasia.

Njoki amekuwa akishiriki Kongamano la Kijamii Duniani tangu lilipoanzishwa katika mji wa Porto Alegre mwaka 2001 nchini Brazil. Njehu anakubali na ukweli kwamba hamasa ilipungua baada ya Kongamano la Kijamii la mwaka 2007, lakini anasema wanachama wa kikundi chao wamebadilisha mtazamo wa ushiriki katika kongamano la WSF litakalofanyika Nairobi.

“Walihamasishwa kuelewa kwamba ushindani ndio njia ya maisha. Haiyumkini kufikiri kwamba maisha ni ushindani wakati wote, kwa sababu mtu anapigania katika kujaribu kupata fedha kwa ajili ya mtoto, suala sio tu ni mtoto bali kupatikanaji wa elimu kwa watoto wote. Iwapo unapigania kupinga mtu anayevuta kinywaji haramu cha gongo (chang’aa)  au bangi katika jamii yako au hupati huduma muhimu kwa sababu una tatizo, kwa mtizamo huo basi sio tu kwa ajili yako, ni kwa ajili ya huduma na hali halisi katika jamii yako.”

Betty Makena Mutugi amekuwa mwenyekiti wa kamati ya wanawake katika Chama Kikuu cha Wafanyakazi  (COTU) kwa kipindi cha miaka minne iliyopita. Alijitahidi kusukuma ushiriki wa wanawake katika ngazi za uongozi kwa wanawake vijana na wenye umri mkubwa katika chama hicho, halikadhalika alipigania haki za mwanamke katika mahali pa kazi. Kongamano la Dakar litakuwa la kwanza kuhudhuriwa na Mutugi.

“Nilipoalikwa katika kongamano hili, nilijisikia vizuri upande wangu ili niweze kujitayarisha na kuona vikundi vingine vinafanya nini,” alisema. Mutugi atakuwa mwakilishi pekee kutoka COTU lakini atakutana na vikundi vingine vingi vya umoja wa wafanyakazi barani Afrika na hata kutoka nje, ambao watajiunga kwa pamoja kuongeza nguvu katika mapambano yao.

“Tuna tatizo kubwa la ubinafsishaji na serikali inachukuwa fursa hiyo, kwa kusema kwamba kuna tatizo au mgogoro. Na wakati wanabinafsisha makampuni hayo hutuambia kwamba itabidi pia wapunguzwe wafanyakazi, nendeni nyumbani, na mara wawekezaji wakiwasili na kununua kampuni, wanaleta watu wao.”

Mithika Mwenda ni mratibu wa shirika la Pan-african Climate Justice Alliance, ambalo ni miongoni mwa watayarishaji wa kongamano la awali la Kijamii la Dunia.

“Kama ujuavyo ni vigumu kwa kila mtu kushiriki. Hivyo basi tunajipanga kuhakikisha ni kwa kiasi gani tutakuwa na uwakilishi wa kutosha katika mchakato huu, sio lazima kwenda Dakar, lakini ule moyo wa kulitambua kongamano hilo. Pili, tunaamini kwamba Kongamano la Kijamii la Dunia ni fursa kubwa ya kurekebisha udhalimu uliokuwa ukitendeka dhidi ya watu kwa muda mrefu.”

Anasema kwamba mkutano wa Januari 29 umekonga nyoyo za harakati za kijamii kwa kuleta maelewano katika tofauti za kikabila zilizojitokeza nchini Kenya.

“Tulianza kwa kujiuliza wenyewe, sawa tunakwenda, lakini tunawahusishaje wenzetu katika ngazi ya kitaifa? Je, ni nini tunaenda kufanya?” alisema. “Hamasa za Kongamano la Kijamii la Dunia ni ushiriki wa watu. Ni kujaribu kuangalia ni kwa namna gani wazawa katika ngazi ya chini, jamii ya msituni na maskini, watu wenye ulemavu, vijana na wengine wote wanaweza kushiriki katika siasa za nchi yetu na hata katika ngazi ya kimataifa kwa ujumla.”

“Wakati Wakenya wanaelekea katika Kongamano la Kijamii la Dunia huko Dakar, wanatarajia kubadilishana uzoefu, na kurejea nyumbani na mikakati mipya na habari njema zenye matumaini ambazo tunaweza kuzichukua ili kufanikisha malengo yao kwa ajili ya kuboresha haki katika maisha ya jamii, kama kauli mbiu ya Kongamano la Kijamii la Dunia lisemavyo, “Dunia mpya inawezekana.”

(END/2011)

Share

Leave a Reply

Advertisement - CAIXA

World Assembly of Migrants
TerraViva - 9 February 2011
TerraViva - 9 February 2011   TerraViva - 8 February 2011   TerraViva - 7 February 2011

Key Global Coverage on IPS NEWS

IPSNews Pictures on www.flickr.com
 

			Nnimmo Bassey - Friends of the Earth, Nigeria   
			Seminar on Migration   
			Traders at the WSF   
 

			The People Need to Take Leadership   
			WSF attracts global participation   
			Representatives from Western Sahara at the WSF   
Multimedia content Partners

Flamme d'Afrique     Panos Institute West Africa

World Social Forum