Lula na Wade Katika Kona Mkabala

Posted on 11 February 2011 by admin

Na Koffigan E. Adigbli

DAKAR, Feb 11 (TerraViva) – Dhana ya uliberali iliyoanzishwa katika nchi maskini zaidi haina nafasi katika jamii za kisasa, anasema rais wa zamani wa Brazili, Luiz Inácio Lula da Silva.
Lula, kama ambavyo anajulikana zaidi, alijitokeza pamoja na Rais wa Senegal Abdoulaye Wade katika Kongamano la Kijamii la Dunia mjini Dakar, ambapo anashiriki katika mkutano wa wanaharakati wa kudai dunia mbadala kutoka duniani kote. Lula alitoa hotuba ambapo alionyesha kuwa na matumaini juu ya takwimu za kiuchumi za sasa.

Brazilian president Luiz Inácio Lula da Silva. Crédit: Pepo Petos/WSFTV

Brazilian president Luiz Inácio Lula da Silva. Crédit: Pepo Petos/WSFTV

“Mfumo wa kiuchumi duniani sasa hautajengwa tena na nchi chache zenye uchumi mkubwa,” alisema.

“Katika Amerika Kusini, lakini zaidi ya hapo katika mitaa ya Tunis na Cairo na miji mingi katika mataifa mengine mengi ya Afrika, matumaini mapya yanazaliwa. Mamilioni ya watu wanaibuka kupingana na umaskini ambao unawakabili, dhidi ya kudhibitiwa na madikteta, dhidi ya nchi zao kukubaliana na sera za mataifa yenye nguvu duniani,” alisema Lula.

Pia alitoa wito kwa Afrika kutambua fursa katika bara hilo na mustakabali mzuri ambao unalisubiri bara hilo, lenye wakazi milioni 800 na utajiri wake mkubwa wa ardhi, ambao ungeruhusu kufikia uhuru wake wa uzalishaji wa chakula.

“Kwa muda mrefu, nchi tajiri zimetuona kama watu hatari na watu wenye matatizo, lakini wale ambao wametupatia masomo ya jinsi gani lazima tusimamie uchumi wetu tena kwa mbwembwe kubwa, hawajaweza wao wenyewe kuepuka mgogoro uliotokana na kitovu cha ubepari duniani,” alisema.

Kwa upande wake, Rais Wade kwa uwazi alijiwakilisha kama mtetezi wa uchumi huria. Alikwenda umbali wa kuonyesha kuwa hakubaliani na harakati dhidi ya utandawazi, hata kama anakubaliana nao juu ya wazo lao la kubadili dunia, jambo ambalo linamfanya kukubaliana na haja ya kuleta mabadiliko.

“Naunga mkono uchumi wa soko na wala siyo uchumi unaoongozwa na serikali ambao umeshindwa mahali pengine au karibu katika dunia nzima,” alisema, akiongeza kuwa kwa muda mrefu alikuwa akifanya kampeni ya kuwa na kiti cha Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

“Nyie nyote ambao mko hapa kama mngeunga mkono dhana hiyo, Afrika ingekuwa tayari ina kiti katika Baraza la Usalama. Tangu mwaka 2000, nimekuwa nikifuatilia harakati zenu na bado – samahani kwa kuwa mkweli – nawauliza swali hili: mmefanikiwa katika kubadili dunia katika ngazi ya kimataifa?”

(END/2011)

Share

Leave a Reply

Advertisement - CAIXA

World Assembly of Migrants
TerraViva - 9 February 2011
TerraViva - 9 February 2011   TerraViva - 8 February 2011   TerraViva - 7 February 2011

Key Global Coverage on IPS NEWS

IPSNews Pictures on www.flickr.com
 

			Nnimmo Bassey - Friends of the Earth, Nigeria   
			Traders at the WSF   
			Seminar on Migration   
 

			The People Need to Take Leadership   
			Representatives from Western Sahara at the WSF   
			WSF attracts global participation   
Multimedia content Partners

Flamme d'Afrique     Panos Institute West Africa

World Social Forum