Mapinduzi Siyo Jambo Dogo

Posted on 10 February 2011 by admin

Andrea Lunt anamhoji Mwanaharakati wa Kenya ONYANGO OLOO

NEW YORK, Feb 10 (IPS/TerraViva) – Nyuma ya vichwa vya habari vya makongamano ya kijamii na maandamano ya kutumia nguvu, kupambana na ukandamizaji na kubadili dunia kunahitaji hatua endelevu zinazojikita katika jamii ya chini, kulingana na mwanaharakati wa haki ya kijamii wa Kenya.

Wakati Kongamano la Kijamii la Dunia mwaka huu likifanyika kikamilifu, IPS ilizungumza na Oloo, mwandishi, mfungwa wa kisiasa wa zamani na mratibu wa taifa wa WSF wa mwaka 2007, kuhusu nchi yake ya Kenya, maandamano yanayoendelea Kaskazini mwa Afrika na vuguvugu la kijamii duniani kote. Sehemu ya mahojiano inafuata.

Courtesy of Onyango Oloo.

Courtesy of Onyango Oloo.

Swali: Umepata nini katika maandamano yanayojitokeza katika eneo zima la Afrika Kaskazini? Ni kwa nini yanajitokeza sasa na unaamini kuwa yanaweza kusambaa katika kanda nyingine katika bara?

Jibu: Ninahamasishwa na kuvutiwa na kile kinachojitokeza nchini Misri na Tunisia. Mapinduzi yanaongezeka, kinyume na matangazo ya vyombo vikuu vya habari, yanatofautiana mno na birika la chai linalochemka ghafla.

Kinachojitokeza leo hii katika Afrika Kaskazini ni ushahidi wa harakati, ushindi na kurejea nyuma ambako kumejitokeza kwa miongo mingi na ni chanzo cha migogoro mingi mno ya kijamii – bila kujali kukosekana kwa muunganiko kati ya uundwaji wa ubeberu wa uliberali wa kisasa na mahitaji makubwa ya demokrasia, haki ya kijamii, amani na jamii bora.

Mapinduzi kwa asili yake siyo bidhaa zinazozalishwa kutoka kiwandani ambazo zinaweza kusafirishwa katika mfumo wa “shinda nishinde” katika nchi nyingine. Hata hivyo, nguvu ya mfano inapaswa kuwa kichocheo kwa ajili ya harakati nyingine za ukombozi wa kitaifa katika Afrika nzima na Mashariki ya Kati.

Swali: Kwa maoni yako, ni vuguvugu gani za kijamii zinazojitokeza nchini Kenya wakati huu?

Jibu: Hili ni swali gumu, kama siyo vigumu kulijibu. Kwanza, mtu hawezi kuweka vuguvugu za kijamii katika aina yoyote ile ya ukiritimba wa “umuhimu” nchini Kenya. Jambo la pili, na kuwa muwazi zaidi,  vuguvugu la kijamii nchini Kenya bado kwa kiasi kikubwa, ni dhaifu mno na wanaharakati wengi wako katika hatua ya uchanga.

Baadhi yao wamekamatwa na NGOs zinazopata ufadhili kutoka Magharibi ili ajenda zao zitekeleze vipaumbele vya wafadhili wa Amerika Kaskazini na mashirika ya wafadhili ya Ulaya.

Hata hivyo, naweza kutaja Bunge la Mwananchi kama shirika lililofanya kazi nzuri katika kusumbua hali ya ukoloni mamboleo.

Swali: Ni aina gani ya mafanikio au mifumo mbadala ya maendeleo nchini mwako, au katika Afrika kwa ujumla, ambayo yanaweza kuhamishiwa katika maeneo mengine ya dunia?

Jibu: Kuna maarifa mengi mno ya jadi ambayo mara nyingi “yanadhoofishwa” na vyombo vya habari vya Magharibi. Nazungumza kuhusu hifadhi ya maarifa ya jadi katika eneo la miti shamba na madawa ya jadi. Katika miaka michache iliyopita hata makampuni makubwa ya madawa yanakubali kuwa aina mbadala za afya ya jadi imeleta mifumo ya afya katika kushughulikia maladhi na magonjwa kama kisukari, magonjwa ya moyo, kansa ya kibofu, kifua kikuu na VVU/UKIMWI.

Rwanda imeonyesha njia ya kushughulikia amani na migogoro kupitia mahakama yake ya gacaca iliyoanzishwa baada ya mauaji makubwa ya kimbari katikati mwa miaka ya 1990.

Wakulima wa Afrika, kama ilivyo kwa wenzao wa Asia, wana njia bora zaidi za kuhifadhi mazingira na kuhifadhi maarifa ya mbegu tofauti na inavyofanya Monsantos ya dunia.

Kwa maoni yangu, wenzangu wa Kenya kutoka eneo linalozungumza lugha ya Maa wameonyesha ujasiri katika kushika utamaduni wao bila kuendeshwa na historia ya masalia yaliyohifadhiwa katika makumbusho.

Credit: Advocacy Project

Umoja Peace Village. Credit: Advocacy Project

Wanawake wa Afrika, kama wanawake wa Umoja Peace Village karibu na Nanyuki katikati mwa Kenya, wamekuja na mifumo ya kuwapatia uwezo wanaharakati wa kijinsia unaotokana na ukweli halisi kama watu wa kijijini, makabila ya ufugaji ya watu wachache – mshtuko kwa wale ambao wana imani kuwa harakati za kijinsia Afrika zinatumika mijini, kwa ajili ya wanawake wenye elimu ya chuo kikuu.

Swali: Ni njia gani bora ya wanaharakati wa kijamii kufanya sauti zao kusikika na kuhakikisha kuwa mawazo yanayojadiliwa katika makongamano kama ya WSF yanatafsiriwa katika ukweli wa mabadiliko ya kisera katika ngazi za kitaifa na kimataifa?

Njia bora ya kufanya sauti zao kusikika siyo kusubiri matukio ya mwaka na vipindi vya Kongamano la Kijamii la Dunia. Tunazungumza vizuri kwa kuwa na ufahamu, tukiwa tumeungana, wenye nguvu na kuwa na hatua endelevu ya kisiasa katika ngazi ya mitaa, kitaifa na ngazi ya bara.

Ninachokisema kwa maneno mengine ni kwamba wanaharakati wasijikusanye tu mbele ya sauti nzuri za taarifa za habari za CNN, BBC, Al Jazeera au hata naweza kusema IPS, lakini kusikiliza dada zao na kaka wanaozungumza nao majumbani, katika jumuiya za mitaa na katika nchi zao wakati wakichambua na kujipanga kukabiliana na aina maalum ya ukandamizaji wao na changamoto.

Kwa njia hiyo, wakati wanaelekea maeneo kama Dakar na Porto Alegre, wenzao kutoka maeneo mengine ya dunia watakachotaka kusikia ni sauti zenye nguvu kutokana na harakati zao wenyewe nyumbani kwao.

Kwa bahati mbaya, sikwenda Dakar mwaka huu kwasababu sikuwa na fedha zozote zile za kupanda ndege kwenda Senegal. Wanaharakati wengi katika Afrika walikabiliwa na changamoto hii. Ni kumbukumbu ya kusikitisha ya vikwazo vinavyotokana na tabaka vya kushiriki katika matukio kama Kongamano la Kijamii la Dunia – hata kama yanafanyika katika bara ambalo tunaliita nyumbani.

(END/2011)

Share

Leave a Reply

Advertisement - CAIXA

World Assembly of Migrants
TerraViva - 9 February 2011
TerraViva - 9 February 2011   TerraViva - 8 February 2011   TerraViva - 7 February 2011

Key Global Coverage on IPS NEWS

IPSNews Pictures on www.flickr.com
 

			Nnimmo Bassey - Friends of the Earth, Nigeria   
			Traders at the WSF   
			Seminar on Migration   
 

			The People Need to Take Leadership   
			WSF attracts global participation   
			Representatives from Western Sahara at the WSF   
Multimedia content Partners

Flamme d'Afrique     Panos Institute West Africa

World Social Forum