Miaka 11 ya Migogoro Migumu Kutatua Kimataifa

Posted on 10 February 2011 by admin

Mario Osava

Credit: Ansel Herz/IPS

RIO DE JANEIRO, Feb 10 (IPS) – Uliberali wa kisasa na utandawazi wa kifedha ni maadui maarufu ambao waliunganisha na kukusanya wanaharakati ambao walianzisha, miaka kumi iliyopita mjini Porto Alegre kusini mwa Brazili, Kongamano la Kijamii la Dunia (WSF) kama nafasi ya kukutana, kutathmini na kujadili, chini ya kaulimbiu “Ulimwengu Mwingine Unawezekana”.

Lakini katika miaka yake 11 tangu kuanzishwa, kongamano la WSF linakusanyika tena Feb. 6-11 mjini Dakar, Senegal, wakati ambapo uliberali wa kisasa, sera za soko huria vinasimama katika ulimwengu unaotishiwa na kuporomoka kutokana na mchanganyiko wa migogoro: ya kifedha, mabadiliko ya tabia nchi, chakula na maji.

Ubeberu wa Kimarekani, shabaha nyingine ya wanaharakati, umeshuhudia nguvu yake ya kiuchumi ikidhoofika wakati taifa jingine lenye nguvu, China, linaibukia na aina yake ya ukoloni, pamoja na kwamba haitumii mbinu za kijeshi au kusafirisha mfumo wake inaoamini na mtindo wake wa maisha – kwa sasa.

Kukua kwa nchi zinazoibukia kiuchumi kumefanya mamia kwa mamilioni ya watu kutoka kwenye umaskini mkubwa. Lakini kukosekana kwa usawa duniani na katika nchi moja moja bado ni doa, kama ilivyo kwa njaa inayokabili watu wengi katika pande nyingi za sayari.

Tishio la mabadiliko ya tabia nchi limeachwa kuongeza idadi ya watu waliokufa na kuhama makazi yao kutokana na matukio ya hali ya hewa, na kuongezeka kwa hasara inayotokana na kilimo.

Fedha zina nguvu kubwa ya kuangamiza, huku kukiwa na dola trilioni 860 zinazokadiriwa kuwa ni mtaji unaozunguka duniani kote – mara 13 zaidi ya Pato la Dunia la Mwaka – kulingana na “Bank of International Settlements”.

Yote hayo yanazidishwa na “utawala mbovu wa sayari” – kukosekana kwa taasisi zenye uwezo wa kushughulika na “matatizo ya kimataifa,” kulingana na mwanauchumi wa Brazili Ladislau Dowbor, ambaye anaelekea Dakar kubadilishana mawazo na kundi la wasomi ambao, chini ya jina la “Migogoro na Fursa”, wanajadili mifumo ya kiufumbuzi ya “mkusanyiko wa migogoro.”

Kuzidi kuongezeka kwa mkusanyiko wa utajiri mahali pamoja ambao umesababisha theluthi mbili ya binadamu kuondolewa katika maendeleo na kuishi kwa asilimia sita tu ya pato la dunia siyo suala endelevu, alisema Dowbor, profesa katika Chuo Kikuu cha Catholic São Paulo.

Wala haiwezekani kuendelea mbele katika “Mazingira haya Makubwa,” na kumaliza maliasili, “ardhi, viumbe wa baharini,” aliongeza.

Waraka muhimu wa kundi hilo la wasomi ambalo ni pamoja na Dowbor, na “mwanauchumi wa jamii” mwenye asili ya Poland na Ufaransa, Ignacy Sachs, na mwanauchumi na mpenda mageuzi wa Uingereza Hazel Henderson, unakataa “maono rahisi ya mchakato wa kutoa maamuzi ya kijamii,” unaotoa wito wa kuokoa “mwelekeo wa taifa la umma,” na kupendekeza kuondokana na GDP kama kiashiria kikuu cha uchumi, miongoni mwa mapendekezo mengine.

Kongamano la WSF linarejea Afrika katika awamu ya nane wakati maandamano ya raia yameshapindua serikali ya kidikteta ya Tunisia na mengine yanatishia kufanya kama hivyo nchini Misri.

Kongamano la mwaka huu “litakuwa zuri, kwa kuwa na watu wapya,” lakini litafanyika katika mazingira hatari, “huku likipata tu theluthi moja ya bajeti iliyokadiriwa hapo kabla,” alisema mmoja wa waanzilishi wa WSF, Cándido Grzybowski, mkurugenzi wa Taasisi ya Uchambuzi wa Kiuchumi na Kijamii Brazili (IBASE).

Katika matukio mengi, kwa mfano, hakutakuwa na watu wanaotafsiri papo hapo.

Baadhi ya washiriki 50,000 wanatarajiwa kushiriki, moja ya tatu ya jumla ya waliojisajili katika kongamano lililopita, lililofanyika mwaka 2009 katika jiji la kaskazini mwa Brazili la Belém katika msitu wa Amazon. “Lakini takwimu hiyo inaweza kuongezeka mara mbili, kutokana na kuongezeka kwa watu kutoka bara la Ulaya,” Grzybowski ana matarajio.

Senegal ina idadi ya watu wachache zaidi mara 15 ikilinganishwa na Brazili, alisema Chico Whitaker, mwanzilishi mwingine wa WSF, ambaye alielezea kuwa asilimia 80 ya washiriki katika matukio haya mara nyingi wanatoka nchi mwenyeji.

Uwepo wa washiriki kutoka Amerika Kusini utakuwa mdogo, kwa sehemu kutokana na matatizo ya kifedha yanayokabi mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutokana na kupungua kwa fedha za wafadhili, kulikozidishwa na viwango visivyokuwa vizuri vya ubadilishanaji wa fedha na uhaba wa ufadhili wa serikali za ndani. Na tiketi za ndege kwenda Dakar zinauzwa kwa gharama kubwa, kutokana na kukosekana kwa ndege za moja kwa moja kutoka Amerika Kusini; ndege zinapitia Ulaya.

Mapungufu ya maandalizi mjini Dakar yanaonyesha kukosekana kuungwa mkono na serikali, kutokana na msimamo uliochukuliwa na mmoja wa wanaharakati wa sasa wa Brazili ambaye aliandaa kongamano mwaka jana kaskazini mashariki mwa Brazili katika jimbo la Bahia na ambaye alitetea ushirikiano na serikali zenye maendeleo, kuimarisha matukio ya WSF na kuyafanya kuwa na faida kubwa.

Kongamano la WSF linafasiliwa kama mpango wa kijamii ambapo viongozi wa serikali wanashiriki tu kama wageni katika matukio yanayoandaliwa na wanaharakati na mashirika ya kijamii. Hata hivyo, makongmano mengi ya kijamii ya dunia, ikiwa ni pamoja nay ale matano yaliyofanyika nchini Brazili, wamepata msaada wa kifedha kutoka serikali za kitaifa au za mitaa.

Rais wa zamani wa Brazili Luiz Inácio Lula da Silva, mgeni mwalikwa katika makongamano yaliyopita, sasa atashiriki katika kongamano la Dakar kama “mjumbe kutoka mashirika ya kiraia “katika semina ya Jumamosi Feb. 7, siku ya Afrika na Waafrika Wanaoishi nje ya Bara katika ratiba ya WSF 2011.

Lula ametangaza kuwa mahusiano baina ya Brazili na Afrika itakuwa kipaumbele katika shughuli zake baada ya kuondoka serikalini.

Wabrazili wengi wanataka kurejesha WSF katika ukumbi wake wa zamani wa Porto Alegre, wakati wengine wanashinikiza kufanyika Bahia, jimbo lenye watu wengi wenye asili ya Afrika.

Lakini Ulaya, eneo jingine lenye nguvu linaloweza kuwa mwenyeji wa kongamano lijalo mwaka 2013, inajikita katika mifumo mingine, kama vile kujaribu kuwa na matunda katika masuala makubwa ya sasa.

Hata hivyo, ni mwelekeo mpya wa “dunia nyingine” ijayo, zaidi ya changamoto za sasa, ambazo zinatia wasiwasi kwa waanzilishi wa WSF. “Maendeleo ambayo yanaua maisha ya watu katika sayari ni tatizo kubwa,” alisema Grzybowski, ambaye alisema kuwa “uchumi wa kijani” kama ufumbuzi, akisema ni “ubepari uliotiwa kijani” ambao hauongezi tija katika mifumo ya mkakati huo.

Mapendekezo yake ni “kwenda zaidi ya WSF” na kutumia fursa ya Rio+20 ya mwaka kesho, Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo Endelevu, ambao utaleta taarifa mpya zaidi na mjadala ulioanzishwa mwaka 1992 katika Mkutano wa Kilele wa Mazingira wa Rio de Janeiro.

Vuguvugu la kijamii linatakiwa kujipanga na kuwepo kwa wingi kwa wanaharakati katika mkutano wa mwaka 2012, ili kujenga ushirikiano na serikali ya Brazili kwa ajili ya kubadili jinsi mazingira na maendeleo yanapaswa kuwa, alisema.

Matatizo ya kimataifa ni mengi na magumu, lakini “dunia haiishii hapo, na watu wanapaswa kujenga historia,” kama inavyoonekana katika ulimwengu wa Waarabu katika siku chache zilizopita, alisema.

(END/2011)

Share

Leave a Reply

Advertisement - CAIXA

World Assembly of Migrants
TerraViva - 9 February 2011
TerraViva - 9 February 2011   TerraViva - 8 February 2011   TerraViva - 7 February 2011

Key Global Coverage on IPS NEWS

IPSNews Pictures on www.flickr.com
 

			Nnimmo Bassey - Friends of the Earth, Nigeria   
			Seminar on Migration   
			Traders at the WSF   
 

			The People Need to Take Leadership   
			Representatives from Western Sahara at the WSF   
			WSF attracts global participation   
Multimedia content Partners

Flamme d'Afrique     Panos Institute West Africa

World Social Forum