‘Ni Dalili za Mabadiliko’ Asema Morales wa Bolivia Wakati wa Uzinduzi wa Kongamano

Posted on 07 February 2011 by admin

Na Thandi Winston na Souleymane Faye*

Kutoka kwa: Abdullah Vawda/IPS

Kutoka kwa: Abdullah Vawda/IPS

DAKAR, Feb 6  (IPS)  РMakumi kwa maelfu ya watu waliandamana katika mitaa ya mji mkuu wa Senegal wa Dakar siku ya Jumapili kuashiria mwanzo wa Kongamano la Kijamii la Dunia linalofanyika kila mwaka. Wanaharakati walibeba mabango ya rangi  mbalimbali yanayokemea upokonyaji wa ardhi, sheria kali za uhamiaji, ruzuku katika kilimo barani Ulaya na Marekani na masuala mengine mengi.

Wengine waliimba nyimbo za uhuru na kupiga ngoma wakati wakiandamana kwa amani kupita katika mitaa kwenye njia inayoanzia karibu na ofisi za shirika la utangazaji la serikali ya Senegal, RTS, na kuishia katika Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop, ukumbi mkubwa wa mkusanyiko huo.

Rais wa Bolivia Evo Morales, ambaye alishiriki katika maandamano, alikaribisha marais wenzake kutoka nchi maskini kushiriki katika tukio hilo.

“Ni lazima kuwepo na uhamasishaji ili kukomesha ubepari na kuwasafisha kabisa wavamizi, wakoloni mamboleo na mabeberu [...] naunga mkono maandamano ya raia nchini Tunisia na Misri. Hizi ni dalili za mabadiliko,” alisema Morales, kiongozi wa zamani wa chama cha wafanyakazi ambaye ni mshiriki wa mara kwa mara katika mikusanyiko ya harakati za kupinga utandawazi.

“Ni lazima kuwepo na upinzani na uhamasishaji. Ni lazima kuwepo na mpango wa harakati za kijamii kujenga dunia mpya,” alisema.

“Ni lazima kuokoa ubinadamu, na kwa kufanya hivyo, ni lazima kuwajua maadui wetu. Maadui wa watu ni wakoloni mamboleo na mabeberu. Ni lazima tukomeshe mfumo wa kibebari na kuweka mfumo mwingine katika nafasi yake. Ni vema kuondokana na matajiri na kubadili dunia.”

Meya wa jiji la Dakar alikaribisha washiriki, lakini wajumbe wengine waandamizi wa serikali ya Senegal hawakushiriki; Rais Abdoulaye Wade mwenyewe yuko nje ya nchi, pamoja na kwamba amepangwa kushiriki katika tukio hilo akiwa na mwenzake wa Brazili baadaye katika wiki.

Kongamano la Kijamii la Dunia linajifasili kama nafasi ya wazi ambapo wale “wanaopingana na uliberali wa kisasa na dunia inayoongozwa na mtaji au aina yoyote ile ya ubeberu wanakuja pamoja kutoa maoni yao.”

Katika tukio la mwaka huu lililofanyika mjini Senegal, mijadala mingi itajikita katika kile ambacho waandaaji wanakitaja kama mgogoro wa ustaarabu na ubepari unaoiandama Afrika na maeneo mengine ya dunia.

“Kongamano hili lazima lichangie katika kuibadili dunia. Ni fursa kwa wale wote ambao wanawakilisha wanaokandamizwa duniani kuzungumza sasa,” alisema mwanahistoria wa Senegal Boubacar Diop Buuba, ambaye ni profesa katika Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop.

Philip Kumah, mfanyakazi wa kijamii nchini Ghana ambaye anafanya kazi katika shirika la Amnesty International, alisema, “Tunataka kukomeshwa kwa ukiukwaji wa haki katika nchi yetu ambayo serikali inawaibia wananchi ardhi. Kongamano hili ni nafasi kwa serikali zetu kuwa na sikio linalosikiliza malalamiko yetu.”

Kwa mwanaharakati Beverley Keene, kutoka Buenos Aires, kufanya kongamano hilo barani Afrika ni mwanzo muhimu. “Ni wakati wetu kujifunza kutoka kwa wengine na kutathmini madhara katika maisha ya jamii ambayo yametokana na mgogoro wa kifedha na uporaji wa madini ya wananchi.”

Mgogoro wa kifedha ni maarufu miongoni mwa kaulimbiu ambazo zitajadiliwa katika kongamano la siku sita ambalo linatafuta njia mbadala ya kukabiliana na “mgogoro uliotokana na mfumo wa kibepari.”

Mwanaharakati wa jinsia wa Italia Sabrina Viche alisema tukio hilo pia ni fursa ya kusikiliza wanawake wa Afrika. “Nimekuja hapa mjini Dakar kuunga mkono wanawake wote wa Afrika, ambao wanaendeleza harakati za kuhakikisha kuwa sauti zao zinasikika, nataka kusikia kutoka kwao harakati zao ni zipi na jinsi gani sisi wa Kaskazini tunaweza kuwasaidia.”

Lakini haijitoshelezi kukutana tu, Canet Raphael, mwanasosholojia kutoka Montr√©al, Canada, aliiambia IPS. “Lazima watu watambue kongamano la kijamii ni nini. Moyo wa Kongamano la Kijamii unatokana na mizizi kutoka vuguvugu la watu katika ngazi ya chini ya jamii.”

Thierry Tulasne, ambaye anafanya kazi inayohusu masuala ya uhamiaji kwenye shirika la Canada alisema, “Sina uhakika kuwa vuguvugu la kijamii linaweza kubadili dunia katika siku za karibuni. Lakini nina uhakika kwamba tone moja la maji linawezekana kuja kuwa mito mikubwa.”

(END/2011)

Share

Leave a Reply

Advertisement - CAIXA

World Assembly of Migrants
TerraViva - 9 February 2011
TerraViva - 9 February 2011   TerraViva - 8 February 2011   TerraViva - 7 February 2011

Key Global Coverage on IPS NEWS

IPSNews Pictures on www.flickr.com
 

			Nnimmo Bassey - Friends of the Earth, Nigeria   
			Seminar on Migration   
			Traders at the WSF   
 

			The People Need to Take Leadership   
			WSF attracts global participation   
			Representatives from Western Sahara at the WSF   
Multimedia content Partners

Flamme d'Afrique     Panos Institute West Africa

World Social Forum