Categorized | Swahili, WSF 2011

Taasisi za Benki Zinashambuliwa, Bila Kujali

Posted on 06 February 2011 by editor

Na Julio Godoy

BERLIN, Feb 3, 2011 (IPS) – Kongamano la Uchumi la Dunia limekuwa uwanja wa watunza fedha katika mabenki mwaka huu kutafuta mbinu za kuendeleza utamaduni wake wa mamlaka. Na kwa mara nyingine, ulikuwa ulingo – tofauti na vile vile kupinga Kongamano la Kijamii la Dunia ambalo linatarajiwa kuanza wiki ijayo katika mji Mkuu wa Senegal, Dakar – ambako madhara makubwa ya utandawazi na yanayotokana na mazingira kutokana na ongezeko lisilozuilika liliachwa kando.

“Tulichokiona Davos ni malipo ya ridhaa yetu wenyewe ya mtaji wa shirika,” Rainer Falk, mtaalam wa uchumi wa utandawazi na mchapishaji wa jarida la wiki lijulikanalo kama ‘World Economy Development’ lililoko Luxembourg, ameliambia shirika la habari la IPS.

“Ni wazi kwamba mbali na madhara yanayoonekana kwa ajili ya utulivu kimataifa na utengamano katika jamii bado kuna msimamo wa fikra za matokeo ya muda mfupi ya kiuchumi katika Kongamano la Uchumi la Dunia (WEF) na mashirika makubwa ya fedha kwa ujumla,” Falk alisema.

Japokuwa WEF inadai kwamba ni mkusanyiko wa watu mashuhuri kiuchumi na kisiasa kutoka nchi zenye viwanda vikubwa, na kama ni hivyo kwa kutumia busara hizo kimataifa, ukweli uliopo ni kwamba ulingo huo haukuona mbali mgogoro wa kifedha na kiuchumi ulioikumba dunia hadi kusababisha madhara makubwa.

Mwaka huu WEF kwa mara nyingine lilipata mshtuko kutokana na uasi uliotumia nguvu katika nchi za Maghreb, ambao ulisababisha kuondolewa madarakani kwa Kiongozi wa Kidikteta wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali na kukaribia ukingoni mwa serikali la Hosni Mubarak wa Egypt.

Mbali na dosari hizo, WEF iliendelea na shughuli zake kama kawaida. Badala ya kuyakabili madhara yaliyotokana na kuporomoka kwa uchumi duniani, na kuhamasisha udhibiti wa kimataifa katika biashara zinazoshukiwa kuzorota, baadhi ya washiriki katika mkutano wa Swiss Alps walitoa wito wa kuacha kuzishambulia taasisi za benki.

Kwa mfano Dimon, Mtendaji Mkuu wa benki ya kitegauchumi ya JP Morgan, alisema kushambulia “si jambo zuri kulifanya.” Dimon aliiambia hadharahuko Davos kwamba ilikuwa ‘dhana kubwa ambayo haikuelewa’ kwamba mabenki yote yalikumbwa na kutokuwa na uwezo wa kulipa wakati huu wa mgogoro wa uchumi.

“Sio kwamba (mabenki yote ya vitegauchumi na fedha za kuzungusha) ziko sawa, sio kwamba watendaji wakuu wote wako sawa. Tunajaribu kufanya kinachowezekana kila siku,” alisema.

Dimon, pamoja na watendaji wakuu wengine wanaoongoza mabenki ya kimataifa, kimsingi walipinga pia marekebisho ya soko la fedha. “Naweza kuthibitisha uwezekano wa mabadiliko baada ya yaliyotokea,” Dimon alisema. “Lakini kushauri kwamba tunatakiwa kuinama na kukubali kwa sababu tunatunza fedha – hilo halikubaliki, sio haki.”

Mabenka waliohudhuria katika WEF huko Davos waliezea wasiwasi wao kuhusu mapungufu makubwa ya umma yanaweza kusababisha hali ya mgogoro wa kifedha kurudia tena, na kutoa wito kwa masharti makali katika mipango na kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha za umma.

WEF halikadhalika unaendelea kupuuza matatizo ya kwamba kuongezeka kwa joto duniani kunaweza kusababisha kusitishwa kwa shughuli za kiuchumi. Badala ya kutoa vivutio kwa vyanzo vinavyobuni nishati na kufikiria mifano mbadala ya uchumi, mijadala ya WEF inagusia tu masuala ya ufanisi wa ekolojia kwa uchache sana.

Falk anasema kwamba WEF imeshindwa kuzungumzia masuala muhimu. “WEF limejitosheleza lenyewe na baadhi ya maneno kuhusu ufanisi wa ekolojia. Bila shaka, washiriki wengi katika mkutano huo wa  Davos aidha bado wanaamini kwamba kuongezeka kwa joto kunaweza kuzuiwa kwa kupunguza baadhi ya mifumo, au wanakwepa ukweli uliopo.”

Kerstin Sack, mratibu wa Kikundi cha ATTAC  kutoka Ujerumani, alisema kwamba WEF imeshindwa kufikia maazimio yanayohusu “matatizo muhimu ya maisha yetu, hususan uhaba wa chakula, ukiukwaji wa kijamii kimataifa na migogoro ya kimataifa inayohusiana na malighafi.”

Sack amesema kwamba kauli mbiu ya mkutano wa WEF mwaka huu imepotosha. Mkutano ulikusanyika chini ya bango lililoandikwa ‘Miongozo ya Pamoja kwa Dunia Mpya’. “Lakini watu waliofika katika mkutano huo Davos hawako tayari kukubali kwamba miongozo ninawafaa wote,” Sack ameliambia IPS.

Sack pia ameshutumu miito iliyotolewa na watendaji wakuu wa mashirika ya kimataifa benk za vitegauchumi na fedha zilizokusanywa huko Davos zimepunguza kwa kiasi kikubwa hasara kwa umma.

“Huu ni ukomo wa unafiki wa shirika,” Sack amesema.  ”Viongozi hao hao wa makampuni walionusurika kuporomoka kutokana fedha za walipa kodi hivi sasa wanatoa wito wa kuongeza makato katika huduma za kijamii.”

Upuuzi wa WEF unapingana na mwelekeo wa kongamano jingine la kimataifa, hususan Kongamano la Kijamii la Dunia (WSF) – ambalo litaanza wiki ijayo katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Wakati washiriki katika kongamano la WEF wanarudi katika shughuli zao za kawaida za sera, WSF itakuwa ikijadili masuala muhimu ambayo Watendaji Wakuu wa kongamano la Davos imedharau – nayo ni uhaba wa chakula, mabadiliko ya hali ya hewa na ukoloni mamboleo.

(END)

Share

Leave a Reply

Advertisement - CAIXA

World Assembly of Migrants
TerraViva - 9 February 2011
TerraViva - 9 February 2011   TerraViva - 8 February 2011   TerraViva - 7 February 2011

Key Global Coverage on IPS NEWS

IPSNews Pictures on www.flickr.com
 

			Nnimmo Bassey - Friends of the Earth, Nigeria   
			Seminar on Migration   
			Traders at the WSF   
 

			The People Need to Take Leadership   
			Representatives from Western Sahara at the WSF   
			WSF attracts global participation   
Multimedia content Partners

Flamme d'Afrique     Panos Institute West Africa

World Social Forum