Wanawake na Watoto wa ‘Afrika’ Ni Waathirika Wakuu wa Migogoro

Posted on 11 February 2011 by admin

Na Thandi Winston

DAKAR, Feb 11 (TerraViva) – Mmoja wa mabinti wanaoongoza Afrika na mwanaharakati wa haki za wanawake, mwanazuoni wa Nigeria Amina Mama anasema wanamgambo wanaopigana wanaenea hasa katika nchi za Sierra Leone na Liberia. Anasema vita na migogoro inaathiri wanawake ambao ni rahisi kuathirika pamoja na watoto wao.

Rape survivor in Malawi's Dzaleka camp for Congolese refugees: every month, seven to ten cases of gender-based violence are reported; few perpetrators are brought to justice. Credit: Kristin Palitza/IPS

Rape survivor in Malawi's Dzaleka camp for Congolese refugees: every month, seven to ten cases of gender-based violence are reported; few perpetrators are brought to justice. Credit: Kristin Palitza/IPS

Mama alikuwa akiongea na IPS pembezoni mwa Kongamano la Kijamii la Dunia kuhusu kuenea kwa wanamgambo wanaopigana katika bara na mjadala wa wanaharakati wa masuala ya wanawake katika kongamano la mwaka huu.

“Wanawake na watoto wamekuwa waathirika wakuu wa migogoro, iwe ile ya baada ya ukoloni au isiwe hiyo, nina imani maslahi ya makampuni yamechochea migogoro,” alisema.

Ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa dhidi ya wanawake wakati wa migogoro umekuwa mkubwa mno. Utafiti wa mwaka 1999 nchini Rwanda kama sehemu ya Mfuko wa Kimataifa wa Wanawake  (GFW) katika mpango wa Kuenea kwa Mapigano ya Wanamgambo, unasema asilimia 39 waliripoti kubakwa wakati wa mauaji ya kimbari mwaka 1994. Asilimia sabini na mbili walisema walijua mtu ambaye alibakwa.

Katika sampuli iliyochukuliwa bila mpangilio maalum ya wakimbizi wanawake 388 wa Liberia wanaoishi katika makambi nchini Sierra Leone, robo tatu waliripoti kudhalilishwa kingono kabla ya kukimbia makazi yao nchini Liberia. GFW ilikuta kuwa zaidi ya nusu walifanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa kingono tangu walipokimbia.

Wastani wa wanawake 50,000 hadi 64,000 walioyakimbia makazi yao walilengwa kudhalilishwa kingono wakati wa vita nchini Sierra Leone.

Mama, ambaye ni mhariri mwanzilishi wa jarida la wanazuoni la harakati za kijinsia la kwanza barani Afrika, ‘Feminist Africa’, kwa sasa ni wenyekiti wa Mfuko wa Kimataifa wa Wanawake, ambao unatoa ruzuku kwa mashirika yanayopigania haki za wanawake duniani kote.

“Kumekuwepo na mabadiliko juu ya kudumu kwa migogoro na vita katika baadhi ya maeneo ya Afrika,” anasema, “Mabadiliko haya yanasababisha aina maalum ya sera na ufuatiliaji na unyanyasaji dhidi ya wanawake. Yanajikusanya jinsi muda unavyosogea.

“Kongo ni mfano mmojawapo, kama ukiangalia unyanyasaji na ubakaji, ulianza wakati wa ukoloni wa Ubelgiji. Hivi ndivyo wanavyofanya kazi.

“Na leo hii wanaume wameiga utamaduni huo wa kutumia vita waliojifunza kutoka kwa wakoloni wa Magharibi.”

Mama kwa sasa anafanya kazi na wanaharakati wa wanawake wa Nigeria, Sierra Leone na Liberia ili kujenga ufahamu wa madhara ya vita kwa wanawake na watoto.

(END/2011)

Share

0 Comments For This Post

1 Trackbacks For This Post

  1. Wanawake na Watoto wa ‘Afrika’ Ni Waathirika Wakuu wa Migogoro | Placedelamode Says:

    [...] Wanawake na Watoto wa ‘Afrika’ Ni Waathirika Wakuu wa Migogoro  » http:// http://www.ips.org [...]

Leave a Reply

Advertisement - CAIXA

World Assembly of Migrants
TerraViva - 9 February 2011
TerraViva - 9 February 2011   TerraViva - 8 February 2011   TerraViva - 7 February 2011

Key Global Coverage on IPS NEWS

IPSNews Pictures on www.flickr.com
 

			Nnimmo Bassey - Friends of the Earth, Nigeria   
			Seminar on Migration   
			Traders at the WSF   
 

			The People Need to Take Leadership   
			Representatives from Western Sahara at the WSF   
			WSF attracts global participation   
Multimedia content Partners

Flamme d'Afrique     Panos Institute West Africa

World Social Forum