SWAHILI

Afrika Habari


TANZANIA: Ufugaji wa Nyuki Wapunguza Umaskini, Watunza Mazingira

DAR ES SALAAM, FEB 15 (IPS) - Ufugaji wa nyuki katika maeneo mengi ya Tanzania unafanyika kuzalisha kipato, lakini kwa jumuiya za pwani, ufugaji huo una madhumuni makuu mawili – kuingiza kipato na kuhifadhi mazingira.

SOMALIA: Ujenzi Upya Katika Vifusi

MOAADISHU, 13 Feb 2012 (IPS) - Magari na mikokoteni ya kusukumwa na punda imeegeshwa huku ikiwa imejaa vifaa, ikiashiria kuwa Wasomali wanarejea, miaka minne baada ya kukimbia nchi yao, huku risasi na mabomu yakiwa yanarushwa katika vitongoji vilivyodhibitiwa na kikundi cha wanamgambo cha Al-Shabaab mjini Mogadishu na hivyo kuzua hofu miongoni mwao.

SOMALIA: Kurejesha Shule Kutoka Mikononi mwa Wapiganaji

MOGADISHU, 13 Feb 2012 (IPS) - Shule zinaanza kufunguliwa tena polepole katika maeneo ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ambazo hadi hivi karibuni zilidhibitiwa na kikundi cha wanamgambo wa Kiislam cha al-Shabaab. Lakini wastani wa asilimia 80 ya wanafunzi bado hawajarejea.

SIERRA LEONE: Kuwatenga Wagonjwa wa Kifafa

FREETOWN, Feb 7, 2012 (IPS) - Alipoanguka kwa mara ya kwanza, Elizabeth Zainab Kargbo alikuwa mwanamke mwenye mafanikio katika umri wake wa ujana, mwenye mimba ya miezi nane na aliyefanya kazi katika sekta ya utumishi wa umma nchini Sierra Leone.

TANZANIA: Kuhamasisha Kilimo cha Embe Kupunguza Madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

DAR ES SALAAM, Feb 6, 2012 (IPS) - Mabadiliko ya tabia nchi yapo kila mahali, ni dhahiri na madhara yake yanajidhihirisha kwa uwazi zaidi kuliko siku za nyuma. Yanaathiri watu kutoka kila sekta na nyanja zote za maisha. Watu wanaoathirika zaidi ni wale wanaoishi katika nchi zinazoendelea hususan katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wake wanategemea kilimo cha mvua.

Kuhamasisha Kilimo cha Embe Kupunguza Madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

DAR ES SALAAM, Jan 26, 2012 (IPS) - Mabadiliko ya tabia nchi yapo kila mahali, ni dhahiri na madhara yake yanajidhihirisha kwa uwazi zaidi kuliko siku za nyuma. Yanaathiri watu kutoka kila sekta na nyanja zote za maisha. Watu wanaoathirika zaidi ni wale wanaoishi katika nchi zinazoendelea hususan katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wake wanategemea kilimo cha mvua.

SUDAN KUSINI: Wanawake Walenga Kulinda Haki Zao Katika Taifa Changa

WASHINGTON, Jan 26, 2012 (IPS) - Wakati Sudan Kusini ikiandaa mustakabali wake wa kiuchumi wa baadaye katika Mkutano wa Kimataifa wa Sudan Kusini (IEC) wiki hii mjini Washington, wanawake kutoka taifa hilo jipya wametoa wito kwa wafadhili kuwekeza katika miradi ambayo inahakikisha kuwa wanawake wanafaidika sawa na mipango ya maendeleo.

‘Fanyieni Kazi Mazungumzo ya Busan’

BUSAN, Korea Kusini, Jan 26, 2012 (IPS) - Watetezi wa haki za wanawake hawajajiandaa kusubiri kutulia kwa vumbi la Jukwaa la Nne la Ufanisi wa Misaada lililomalizika katika mji wa bandari wa Korea Kusini Des. 1 huku wakitaka kuwepo kwa usawa wa kijinsia na uwezeshwaji.

Clinton Ahimiza Ajenda ya Jinsia Huko Busan

BUSAN, Korea Kusini, Jan 26, 2012 (IPS) - Wanawake wanavuja jasho mashambani katika maisha yao yote wakizalisha chakula na kuimarisha uchumi ambao unategemea zaidi kilimo katika bara la Afrika, lakini wakati baba zao, waume au watoto wao wakubwa wa kiume wanapofariki, hawakaribishwi tena katika ardhi ambayo wamekuwa wakilima kwa miaka mingi.

‘Hakuna Lolote Kutoka Busan kwa Wanawake na Watoto wa Afrika’

BUSAN, Korea Kusini, Jan 26, 2012 (IPS) - Pamoja na kuwepo kwa mafanikio katika kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga, mamilioni ya wanawake na watoto barani Afrika wanahitaji huduma bora za afya, chakula na huduma za usafi wa mazingira.

News in RSS

Gulf News Agencies - Swahili Version

UKAID BMZ Aid Program